Wednesday, January 25, 2017

Tafakari kwa Binti kabla ya kuolewa

#NDOTO_ZA_MABINTI_WENGI_NI_HARUSI.
Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi. Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku. Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele. Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.
Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye #HARUSI yake wamchangie.
Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.
Hawajiulizi maswali ya msingi kama;
=> JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?
=> NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?
=> JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE? (Surrendering my will)
=> JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?
=> JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?
=> JE' NIKO TAYARI KUAMBATA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?
*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?
*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?
*Una uwezo wa kubeba majukumu kama Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?
*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?
*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa? Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.
*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo. Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?
Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon. Me nimemaliza.
Kwa usawa huu hakuna mwanaume anataka kuoa mzigo. Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.

Mwanamke akipenda amependa kweli

Mwanamke akipenda anapenda kweli!
Mwanamke akikupenda anakuwa na furaha, anakuwa anajivunia kuwa na wewe, na hujihisi furaha kuongea na wewe.
Hupenda awe rafiki wa rafiki zako na ndugu zako, uvipendavyo na yeye atavipenda, atabadilisha mtindo wake wa maisha kuendana na mtindo wako.
Haitajalisha ni kiasi gani utamuudhi, atakusamehe hata kabla hujamuomba msamaha, atachokifanya ni kusubiri tu umuombe msamaha kuthibitisha kama kweli umejutia kosa lako.
Atajaribu kuwa na wivu na atakulinda kwani atahitaji uwe wake, wake peke yake na sio ku share. Atawakataa wengine wote wanaomtongoza kwa sababu ameona kesho yake ipo mikononi mwako.
Haitajalisha ni kiasi gani uko mbali na yeye, atajilinda kwa ajili yako. Atalike na ku comment kila kitu unachoweka facebook hata kama ni cha kipuuzi (hahaahaa).
Atakujibu kwa wakati text zako either watsapp, za kawaida au inbox ya fb. Hatajali kama unampa pesa au laa, kama ni tajiri au laa kwa sababu lengo lake ni kujenga maisha na wewe na sio kupass time ameona potentials kwako.
Atakuonyesha marafiki zake na ndugu zake, kwa sababu anajivunia kuwa mpenzi wako.
Tafadhali sana, muangalie mwanamke huyo, moyo wake umejawa na mapenzi, anastahili kutunzwa na kupendwa kama almasi.
Lakini tatizo kubwa la hawa "wavulana" (baadhi yao) baada ya kumfanya akupende zaidi, baada ya kupoteza muda wake juu yako, baada ya kuwakataa wanaume wengine ambapo kimsingi wengine walikuwa tayari kumuoa, baada ya kumuacha akutambulishe kwa ndugu zake na marafiki sasa unamuacha, unamkataa kwa mbwembwe nyingi, unamuacha akiwa na maumivu na aibu kubwa kwamba atawaambia nini wazazi wake, ndugu na marafiki, atatambulisha wangapi?
Na akiulizwa yuko wapi yule uliyetutambulisha? Awajibu nini!? Ofcoz atakachofanya ni kuinamisha kichwa huku ameshika mashavu! Hana jibu ni aibu na maumivu makubwa kwa kuwa alikupenda kwa dhati.
Mbona mnawaweka katika wakati mgumu wanawake waliopewa moyo wa kupenda?
Brothers, usimfanye mwanamke wako ajute kwanini alipenda, usifanye wengine wamcheke na kumdhihaki. Timiza ahadi yako, kama amekukosea na kukuomba msamaha jaribu kumpa nafasi ya pili. Kila mtu anahitaji nafasi ya pili ili aweze kurekebisha pale alipokosea.
Na nyie vijamaa mnaokua sasa, miaka 14 na kuendelea msiige tabia ya sisi kaka zenu, hiyo sio tabia njema kabisa. Jifunzeni kuheshimu hisia za mtu. Kujeruhiwa kihisia kunauma kuliko maumivu ya risasi.
Kama huna future nae usimtongoze na kumpa mimba

Jinsi ya kujikinga dhidi ya magonjwa haya ya zinaa

Njia bora na ya uhakika zaidi kwa wasichana kujikinga dhidi ya maambukizo ya magonjwa ya ngono ni kuachana na ngono katika umri mdogo na kabla ya ndoa. Uelewa juu ya magonjwa haya pia ni njia inayosaidia katika mapambano.
Kwa wasichana ambao hawajaanza kujamiiana na wanaume, wanaweza kupewa chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa wa saratani ya mlango wa mji wa mimba ambayo ni salama. Chanjo hii haiwasaidii wasichana ambao tayari wamekwishaanza tabia ya kujamiiana na wanaume katika umri mdogo kwa vile mara nyingi huwa wamekwisha pata maambukizi.
Njia pekee inayosaidia wasichana ambao wamekwishaanza kujihatarisha kwa kufanya ngono mapema, ni kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika vituo vya tiba za kisayansi ili kuona kuwa viashiria vya awali vya saratani vimeanza kujitokeza au la.
Uchunguzi huu hufanyika kwa kutumia kipimo cha mpako wa asidi ya Acetic na kuangalia - Viasual Inspection with Acetic Acid (VIA). Kama itagundulika kuwa msichana tayari amekwisha athirika kwa virusi hawa, atapatiwa matibabu kabla hajachelewa. Saratani ya mlango wa mji wa mimba inazuilika na kutibiwa kabisa iwapo itagunduliwa na kutibiwa mapema.
Tabia ya kuchangia nguo za kuvaa au taulo za kujifutia maji baada ya kuoga pia ikiepukwa, inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kinga ya magonjwa haya. Magonjwa kama kaswende, kisonono, upele na mengine yanaweza kuambukizwa kwa urahisi kupitia njia hii ya kuchangia nguo, mavazi ya aina nyingine au matandiko.
Njia nyingine ya muhimu ni ile ya kuepuka vishawishi kutoka kwa wavulana na wanaume wasiojiheshimu. Vishawishi vya pesa, simu za mkononi, lifti za magari, vyakula kama viazi vya kukaanga maarufu kama chips na nyama ya kuku, mara nyingi hutumika kuwanasa wasichana wengi hasa wale wenye tamaa mbaya ya vitu na wenye uroho wa vyakula. Wengi husahau umuhimu wa maisha na masomo na huangalia vishawishi kama mafanikio, badala ya mtego yenye hatari kwa afya zao na maendeleo yao.
Kumbuka kuwa mazoea mabaya yakisitawishwa ni vigumu sana kuyaacha. Jitihada kubwa sana zinahitajika ili kuepuka mtego huu wa kufanya mapenzi na ngono katika umri mdogo. Jitahidi kwa kadri ya uwezo na nguvu zako zote za kimwili, kiroho na kiakili kupambana na hisia hasi kuelekea ngono hata kama ni vigumu, kwani huo ndio uamuzi sahihi na salama.
Jaza mawazo na hisia njema katika akili yako kila siku na kuepuka jambo lolote linalokupeleka katika mtego wa kuwazia mapenzi ya mahaba na ngono.Tamaa ya ngono inaweza kutawaliwa kwa mafanikio, kwani Mungu ameweka uwezo mkubwa ndani ya akili za wasichana ili waweze kujitawala. Na ushahidi wa jambo hili ni mwingi sana katika jamii za mataifa mbalimbali katika historia.
Epuka hadithi na liwaya za mahaba, magazeti ya udaku yanayosifia ngono, vipindi vya luninga (Televisheni) vinavyopamba mambo ya mapenzi na ngono kiufundi ili kuwavutia vijana. Epuka mitandao ya wavuti pamoja na mikanda ya video inayoonyesha picha za ngono na miziki inayochochea mapenzi na ngono. Nijambo la busara pia kuwaepuka marafiki pamoja na vijana wa rika lako wasiokuwa na maadili mema.
Wasichana wengi huondoa hofu na kujidanganya kuwa wanaweza kuonyeshana mapenzi na wavulana kwa kukumbatiana, kubusiana, kunyonyana ndimi na kushikanashikana sehemu za siri bila kufanya ngono. Hilo ni jambo la hatari, ni mbegu nzuri ambayo baada ya muda mfupi itazaa matunda ya ngono hatarishi.
Matendo hayo huamusha na kuchochea kwa nguvu sana hisia, tamaa mbaya na hamu kali ya ngono kwa wasichana na wavulana ambayo itawasumbua sana na baada ya muda mfupi sana watatumbukia ghafla katika mtego wa ngono hatarishi. Kanuni ya usalama ni kuepuka kuchezacheza na mambo ya hatari. Epuka kuchezacheza na bunduki yenye magazini iliyojaa risasi, kwani ni rahisi kufyatuka na kusababisha maafa makubwa.

Athari za magonjwa ya ngono kwa wasichana

Wasichana wengi wanaojihusisha na maswala ya ngono katika umri mdogo wanakabiliwa na ongezeko la uwezekano wa kupata saratani ya mlango wa mji wa mimba (cervical cancer). Shingo ya mlango wa mji wa mimba ambayo haijakomaa inapokutana na misukosuko ya ngono hudhoofika na kupoteza nguvu za kukabiliana na mashambulizi ya virus vya Human Papilloma – (HPV) ambao husababisha saratani hiyo mapema au baadaye sana.
Virusi hawa huambukiza kwa njia ya kujamiiana na wanaume hata kama mwanaume atakuwa amevaa kondomu wakati wa kufanya tendo la ngono na msichana. Saratani hii ni tatizo kubwa la kiafya linaloongoza kwa vifo vya wanawake vitokanavyo na ugonjwa wa saratani katika nchi zinazoendelea. Saratani hii kwa kawaida huwapata wanawake wengi ambao huanza kufanya tendo la kujamiiana katika umri mdogo, miaka michache baada ya kuvunja ungo.
Wasichana na wanawake wenye wapenzi wengi, au wenye wapenzi wa kiume ambao wana mtandao mkubwa wa wapenzi wengine wengi, huwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa bahati mbaya sana wasichana wengi hupata maambukizi ya virusi hawa kwa kufanya ngono kwa mara ya kwanza, hata kama ni mara moja tu. Tatizo jingine kuhusiana na maambukizi ya virusi hawa ni kwamba, msichana anaweza kuishi na virusi hawa bila habari kwa miaka 10 hadi 15 hivi ndipo madhara yake yanapojitokeza kwa wazi.
Tatizo jingine linalowakabili wasichana wadogo wanaoendekeza ngono ni ugumba wakati watakapo hitaji kuzaa. Magonjwa mengi ya ngono hushambulia mirija ya uzazi na kusababisha mirija hiyo izibe. Mirija ya uzazi inapoziba, hushindwa kupitisha mayai kwa ajili ya kutunga mimba pale msichana atakapohitaji kupata watoto hapo baadaye.
Magonjwa ya ngono kwa wasichana pia husababisha maumivu makali na kuugua hasa pale tumbo la chini linaposhambuliwa. Msichana hupata ugonjwa wa mwanamimba yaani uambukizo katika mji wa mimba na wakati mwingine katika njia ya mkojo. Hii pia huambatana na maumivu makali wakati wa kukojoa.
Magonjwa mengine katika kundi hili la magonjwa mengi mbalimbali, husababisha madhara makubwa na ya muda mrefu. Kaswende inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na akili hasa pale msichana anapochelewa kupata matibabu sahihi. Magonjwa haya pia yanaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili huku yakiendelea kudhuru afya ya msichana.

Magonjwa yanayohusiana na tendo la ngono

Magonjwa ya ngono ni maambukizi yanayosambazwa kwa njia ya tendo la ngono au kujamiiana. Magonjwa haya kwa karne nyingi yamejulikana kama nyororo la maangamizi au bomu la kibaiolojia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ukiona mgonjwa mmoja mwenye tatizo la ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya ngono basi ni muhimu kutambua kuwa kuna mtu mwingine nyuma yake ambaye ana tatizo hilo pia.
Kwa kawaida wasichana huwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa ya ngono kama watajiingiza katika vitendo vya kujamiiana. Sababu kubwa zinazowaweka katika hatari ni ile hali ya kushindwa kuamua namna ya kufanya ngono kwa tahadhari, maumbile ya kike kama mpokeaji na kutokukomaa kwa shingo ya mji wa mimba nazo ni sababu zingine zinazoongeza hatari.
Magonjwa mengi ya ngono husababishwa na bakteria, virusi, kuvu (fungus), protozoa na parasaiti. Magonjwa yasababishwayo na bakteri ni kama vile kisonono, mitoki (Granuloma inguinale na Chancroid), kaswende na klamydia. Magonjwa kama vile malengelenge (Herpes simplex), molluscum contageosum, viotea (warts), virusi vya UKIMWI na saratani ya mlango wa kizazi (HPV infection) haya hutokana na virusi. Magonjwa yasababishwayo na kuvu ni kama vile kandidiasisi ambayo huambatana na muwasho sehemu za siri. Magonjwa yaletwayo na protozoa kama vile Trikomoniasisi pia husababisha muwasho sehemu za siri na hutokwa kwa majimaji machafu yenye harufu mbaya hasa kwa wanawake. Upele na chawa wanaokuwa kwenye nywele za kinenani haya pia ni magonjwa ya ngono yanayosababishwa na parasaiti.
Dalili za magonjwa ya ngono hujitokeza kwa njia na dalili nyingi. Wakati mwingine magonjwa haya hayatokezi dalili zozote na pia mgonjwa anaweza kupata maambukizo ya magonjwa mawili au zaidi kwa wakati mmoja anapotenda tendo la ngono. Hatari kubwa zaidi inayoambatana na magonjwa haya ni kutokuwepo kwa dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa haya kama vile UKIMWI.

NGONO KABLA YA NDOA KWA MSICHANA

Siku hizi ngono kabla ya ndoa hutazamwa na vijana wengi kama jambo la kawaida.Vijana wa kike na wa kiume hawahisi hatia yoyote ya kuwa na uhusiano wa kingono katika umri mdogo. Kwa kufanya hivi vijana hupoteza mwelekeo kwa kuishi kiholela bila ya kuwa na mwongozo unaongoza maisha yenye mafanikio sasa na baadaye. Uwezo, fursa na bahati ya vijana kwa ajili ya maisha bora hupotea bure. Vijana hufikiria kuwa ngono ndilo jibu na ufumbuzi wa hali ngumu wanayokabiliana nayo wakati wa balehe na kupevuka. Wengi wao hupungukiwa uwezo wa kutabili nini kitatokea baadaye kama matokeo ya ngono kabla ya ndoa.
Wasichana wanaojiingiza katika mahusiano ya kingono kabla ya ndoa na katika umri mdogo huweka rehani uaminifu, afya na uvumilivu wao wa hisia kuhusu mahusiano ya kingono wakati watakapo ingia ndani ya ndoa hapo baadaye.Vijana wengi hawaelewi kuwa ngono haramu huzaa wivu, tuhuma mbaya na majanga ya kijamii. Hufanya mwenzi kumfikiria msichana kuwa ana udhaifu wa kimaadili na hali hii hutia alama katika hisia za mwenzi kuhusu hali ya uaminifu wa mwenzake hasa pale anapokuwa mbali naye.
Tafiti kadha wa kadha huonyesha kuwa wasichana wasiothamini umuhimu wa kujitunza, kujilinda na kubakia waaminifu kabla ya ndoa, wana uwezekano mara dufu wa kufanya ngono nje ya ndoa baada ya kuolewa ikilinganishwa na wale wanaojitunza na kuanza ngono ndani ya ndoa. Uzoefu pia unaonyesha kuwa wasichana wengi wanaoanza ngono kabla ya ndoa, maisha yao ya baadae huwa magumu kutokana na kuacha masomo au kuzaa hovyo ovyo bila mpangilio. Wengi hujikuta wakizaa na wanaume wengi tofautitofauti na kusababisha malezi ya watoto kuwa magumu.
Wasichana wengi hufikiri kuwa ngono kabla ya ndoa ndio njia pekee ya kujenga na kudumisha uhusiano wa kimapenzi na wavulana. Hii si kweli na huenda msichana na mvulana wanaotamaniana kingono hutazamana kwa mitazamo inayotofautiana kabisa mara baada ya tendo la ngono. Ni vigumu kutabiri nini kitatokea baada ya mvulana kutosheleza tamaa yake ya ngono kwa mara ya kwanza.
Huenda mvulana akamwona msichana havutii tena kimahaba na kumchukia sana. Huenda msichana pia akapata athari za kisaikolojia na kupata hisia za kunyanyaswa kijinsia au kutumiwa kama chombo cha kustarehesha wanaume kingono. Na huenda akajichukia kwa udhaifu na kujirahisisha aliko onesha. Hii mara nyingi hutokea pale msichana anapokataliwa na mvulana baada ya kupata mimba.
Mbali na athari za kisaikolojia na kijamii, ngono katika umri mdogo kabla ya ndoa pia inazo hatari za kiafya katika mwili wa msichana. Tishio kubwa kwa wasichana ni maambukizi ya magonjwa kama vile virusi vya UKIMWI, kansa ya mlango wa mji wa mimba na magonjwa mbalimbali yaambukizayo kwa njia ya ngono.

Maalum kwa kina Dada: Sheria 10 za Kumridhisha mwanaume wako kimapenzi!

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/03/wowowo.jpg?x41673Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo barabara!
Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani. Sasa swali linakuja…..Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo, Bi. Layla amekuja na sheria 10 zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.
# 1 Vaa vizuri. Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.
#2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. Mwaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.
#3 Fanya mazoezi na onekana Bomba. Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la kumpelekesha kirahisi kitandani, Basi!
#4 Kuwa Mchokozi. Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake.
#5 Jiamini na Jipende. Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.
Usikose muendelezo wa sheria 5 za mwisho juma lijalo………………………….

Mambo ya kuzingatia kabla ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/02/young-couple-in-bed.jpg?x41673
Mapenzi ni moja ya mahitaji muhimu ya wanadamu, kila mmoja wetu ahahitaji kupenda na kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba.
Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvumiliana na kuweza kuishi pamoja ni mkubwa zaidi.
Kwanza ni lengo (ambition), kama mmoja kati wa wapenzi (nazungumzia wapenzi ambao wanampango wa kuishi pamoja kama mke na mume) ni mtu wa kuwa na malengo na anataka kufanya kitu fulani au kuwa mtu fulani katika maisha yake na mwenzake anachukulia siku kama inavyokuja (laid back), huyu ambaye ana malengo atamchukulia ambaye ni “laid back” kama ni mvivu. Wapenzi wanatakiwa wasipishane sana katika malengo yao hata kama wana kazi mbali mbali.
Pili ni uwazi (openness), kama mpenzi wako ni “open minded” anapenda kujifunza vitu tofauti, kujaribu vyakula tofauti, kusafiri n.k. Yule ambaye anapenda kujifunza mambo mapya kila siku atamuona mwenzake anaboa.
Tatu, wapenzi wanaweza kuwa tofauti katika ujuzi wa hisia (emotional intelligence). Hapa kama tofauti sio kubwa, watu wanaweza kuvumiliana na kuishi pamoja, ila kama tofauti ni kubwa sana, yule ambaye hana ujuzi wa hisia, atakuwa anamburuza na kumharibia mudi yule ambaye amesimama imara kwenye mambo ya hisia. Onyo kwa wanaume ambao wana ujuzi au utaalam wa kusoma hisia za wanawake, wanawake ambao wana F katika ujuzi wa hisia huwa wanavutiwa sana na watu kama ninyi.
Nne ni usosho, kama mmoja wenu ni mtu wa watu anapenda kuongea na watu na anamarafiki kibao, utamkwaza ambae ni mtu ambaye anapenda
maisha “private” na ya utulivu. Mwenzako atakuwa bize anaweka picha zenu na status zinazowahusu facebook wakati wewe unataka mambo ya ndani yawe ya ndani tu. Kama tofauti si kubwa sana mnaweza vumiliana kama tofauti ni kubwa, muda si mrefu mtashindwana
Tano ni wivu. Wivu ni kitu kibaya sana, kama mpenzi mmoja ana wivu ni ngumu kuekewana na ambaye hana wivu. Kama wote mna wivu, sawa kwani kila mmoja ataepuka kufanya mambo ambayo yanamuumiza mwenzake, ila kama mmoja ndio ana wivu ataona mwenzake hajali, basi ukimuona mwenzako anaongea na classmate wake wa zamani au ukiona mtu amepiga picha na mpenzi wako ameshikwa bega basi inakuwa fujo tupu. Kama upo tayari kwenye uhusiano, na mwenzako ana wivu, jaribu kumuelewesha kwamba kum-kumbatia rafiki yako sio kwamba ndio una mipango mingine ya siri.
Kikubwa katika yote ni uaminifu, kama hamna uaminifu katika mapenzi au ndoa. Usipasue kichwa, ondoka na tafuta mtu ambaye anakuamini au kama haupo tayari kuwa mwaminifu usijiingize katika mahusiano, utajiumiza mwenyewe na mwenzako. Msome mwenzako kabla ya kuanza kuitana wachumba, kama tangu siku ya kwanza mwenzako ana wasiwasi na wewe ukikaribia simu yake, ni afadhali umuulize mapema, kulikoni? Kama umepoteza uaminifu katika mahusiano yako, usihofu, muonyeshe mweza wako kwamba umebadilika na jinsi muda unavyoenda atajifunza kukuamini tena.
Hizi sifa zilizotajwa hapo juu sio za kina sana, lakini ni moja wapo ya mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wako wa maisha(kama basi mapenzi yana macho) kabla ya kujizamisha katika mapenzi. Je wewe unaona ni mambo gani ya kuzingatia katika mahusiano na ni mambo gani yanasababisha ndoa kuvunjika? Usisite kuandika maoni yako.

Kujinyonga kwa ajili ya mapenzi ni ujinga wa kiwango cha Phd na hauvumiliki

Wikiend hii mitandao ya kijamii ilijaa post inayomhusu kijana mmoja aliyejinyonga kwa ajili ya mdada aliyemtambulisha katika barua yake kama Rose. Kwanza nakemea vikali vijana wenye akili za kihuni kama hizi kufikiria kusalitiwa kwamba remedy ni kujinyonga ni upuuzi wa hali juu.

Mwanamke yoyote ni oppotunistic sio Rose peke ake watu wanajali maslahi ivi kwann mnawapa wanawake kazi ambayo hata wewe ungepewa usingeweza ni nan mwenye uwezo wa kuacha laki moja akachukua elf kumi eti kisa anampenda mwenzie kama tatizo ni pesa na wewe tafuta upate upendeke.
 

Sababu zinazotupa maumivu baada ya kutendwa

Wengi wetu wameshakumbana na maumivu makali na wana madonda nafsini mwao pamoja na majeraha yaliyosabishwa na mapenzi. Haya yote hutokea baada ya wewe kutendwa. Umeshawahi kujiuliza kwanini hutokea hayo?

1.Kuruhusu akili/ubongo wako utawaliwe na Huyo mpenzi wako.
Sikatai najua kuna kupenda na hutokea automatic, lakini unapokuwa katika mapenzi ni kosa kubwa sana kuruhusu ubongo wako kutawaliwa na mpenzi wako.

Mwisho wa siku unajikuta ukimuwaza yeye kwa sehemu kubwa na kumuona yeye ni kila kitu kwako. Wengine huwaona wapenzi wao ndio miungu yao hapa duniani. Hili ni kosa kubwa sana kumbuka yule ni mwanadamu mwenzako mwenye akili na mawazo ya kibinadamu. Muda wote anawaza akawaza vingine juu yako.

2.Kumuamini kulikopitiliza
Usimwamini mtu kwa asilimia mia kwani huwezi kuona au kufahamu akiwazacho.

3.Kutokujiandaa psychologically
Unapokuwa na mpenzi lazima uiandae saikolojia yako pia kwa kuwa inaweza kutokea mkaachana na mkiachana ni jambo la kawaida. Hivyo ikitokea haitokuumiza sana.

Ukiweza kuufundusha ubongo wako juu ya haya basi mapenzi hayatakutatiza sana. Zaidi na zaidi jifunze kumtegemea Muumba wako zaidi ya vyote.
 

Kutendwa ni elimu katika mapenzi usiogope japo inauma.

Moyo huuma sana pale unapotendwa lakini utajifunza kitu kuhusu tabia za watu mbalimbali na matendo yao katika mapenzi hivyo huweka fikira fulani ya kuyatibu na kujazoea mapenzi,usikate tamaa unapotendwa kwani ndio ukubwa na ni elimu tosha katika mapenzi. NOTE: "One yes *Twice not"
 

SHTUKA MREMBO: MAMBO MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUTENDWA NA UMPENDAE.

 
KATIKA MAISHA YA KIMAPENZI HAKUNA KITU KINACHOUMA KAMA KUSALITIWA, TENA KUSALITIWA KUNAKOUMA ZAIDI NI PALE UNAPOBAINI MPENZI WAKO KAMPA PENZI MTU UNAYEMJUA HALAFU UKIJILINGANISHA WEWE NA HUYO ALIYEPEWA UNASHINDWA KUELEWA KILICHOMSHAWISHI MPENZI WAKO KUMPA PENZI HUYO MTU...

Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake.... 
Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? 

Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.
Yafuatayo baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.

Kubaliana na kilichotokea
Kama keshakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.

Usijilaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema “najuta kumkubalia awe mpenzi wangu”. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.

Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempa basi uchukue kisha uufanyie kazi.
 
Pima ulivyoathirika
Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

Mweleze ukweli
Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze ukweli juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.

Chunguza kwa nini kakusaliti
Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.

Usikubali akulainishe
Huenda huyo mpenzi wako ni msanii na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.

Amua kusuka au kunyoa
Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye  kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.

Msamehe
Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani
 
Iwe fundisho kwako
Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakukuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

Je, Niko Tayari Kuanzisha Urafiki wa Kimapenzi?


VIJANA HUULIZA

Je, Niko Tayari Kuanzisha Urafiki wa Kimapenzi?

Urafiki wa kimapenzi ni nini?
  • Ni kawaida kwako kwenda matembezi pamoja na mtu wa jinsia tofauti. Je, huo ni urafiki wa kimapenzi?
  • Unavutiwa na mtu wa jinsia tofauti naye anavutiwa nawe pia. Mara kadhaa kwa siku unamtumia ujumbe mfupi kwenye simu au unampigia simu. Je, huo ni urafiki wa kimapenzi?
  • Kila mara mnapokuwa katika tafrija pamoja na marafiki, unatumia muda mwingi pamoja na mtu yuleyule wa jinsia tofauti. Je, huo ni urafiki wa kimapenzi?
Huenda haikuwa vigumu kwako kujibu swali la kwanza. Lakini huenda ulisita kidogo kabla ya kujibu la pili na la tatu. Urafiki wa kimapenzi ni nini hasa?
Urafiki wa kimapenzi ni urafiki kati ya watu wawili wanaovutiana kimahaba na unatia ndani shughuli yoyote ya kirafiki ambayo wanafanya pamoja.
Kwa hiyo, jibu la maswali yote matatu ni ndiyo. Iwe kwa simu, uso kwa uso, mbele ya watu, au mahali pasipo na watu, ikiwa wewe na rafiki yako wa jinsia tofauti mnaonyeshana mahaba na mnawasiliana kwa ukawaida, basi huo ni urafiki wa kimapenzi.

 Ni nini kusudi la kuanzisha urafiki wa kimapenzi?

Urafiki wa kimapenzi unapaswa kuwa na kusudi lenye kuheshimika, yaani, kumsaidia mwanamume na mwanamke kujua ikiwa wanaweza kufungua ndoa.
Labda vijana wenzako hawauoni urafiki huo kuwa jambo zito. Pengine wanafurahia tu kuwa na rafiki wa pekee wa jinsia tofauti bila kusudi lolote la kufunga ndoa. Huenda hata wengine wao wanawaona rafiki hao kuwa tuzo au pambo ambalo linawafanya waheshimiwe.
Hata hivyo, mara nyingi urafiki huo usio na msingi mzuri haudumu. Msichana mmoja anayeitwa Heather alisema hivi: “Vijana wengi ambao wanaanzisha urafiki wa kimapenzi, wanauvunja baada ya juma moja au mawili. Wanaanza kuwa na maoni ya kwamba urafiki huo ni wa muda tu, na maoni hayo yanawatayarisha kwa talaka badala ya ndoa.”
Ni wazi kwamba unapoanzisha urafiki wa kimapenzi na mtu fulani, hisia zake zinahusika. Kwa hiyo hakikisha kwamba una nia nzuri.—Luka 6:31.
Ukianzisha urafiki wa kimapenzi bila kusudi la kufunga ndoa, utakuwa kama mtoto anayechezacheza na kitu cha kuchezea kisha anakiacha
Jiulize: Je, ungependa mtu fulani achezee hisia zako kama vile mtoto anavyochezacheza na kitu cha kuchezea kisha anakiacha? Basi usimchezee mtu mwingine! Biblia inasema kwamba upendo “haujiendeshi bila adabu.”—1 Wakorintho 13:4, 5.
Msichana anayeitwa Chelsea anasema hivi: “Wakati mwingine ninaona kwamba urafiki wa kimapenzi unapaswa kuwa jambo la kujifurahisha tu, lakini haliwezi kuwa jambo la kujifurahisha tu ikiwa mtu mmoja anauchukulia urafiki huo kwa uzito naye yule mwingine anauona kuwa mchezo tu.”
Dokezo: Ili ujitayarishe kwa ajili ya kuanzisha urafiki wa kimapenzi na ndoa, soma 2 Petro 1:5-7 na uchague sifa moja ambayo unapaswa kufanyia kazi. Baada ya mwezi mmoja, chunguza uone umejifunza kuihusu kwa kadiri gani na umeifanyia kazi kwa kadiri gani.

 Je, nina umri wa kutosha kuanzisha urafiki wa kimapenzi?

  • Unafikiri ni umri gani unaofaa kijana kuanzisha urafiki wa kimapenzi?
  • Sasa mwulize mmoja wa wazazi wako swali hilohilo.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba jibu lako limetofautiana na la mzazi wako. Au labda majibu yanafanana! Huenda ukawa kati ya vijana wengi ambao kwa hekima wanasubiri kuanzisha urafiki wa kimapenzi hadi watakapokuwa na umri wa kutosha kujielewa vizuri zaidi.
Hivyo ndivyo Danielle, mwenye umri wa miaka 17 alivyoamua kufanya. Anasema hivi: “Nikifikiria jinsi nilivyohisi miaka miwili iliyopita, sifa ambazo ningependa mtu ninayetaka kufunga ndoa naye awe nazo ni tofauti sana ninapolinganisha na zile ninazoangalia sasa. Kwa kweli, hata sasa sioni kama ninaweza kufanya uamuzi mzuri kuhusu hilo. Ninapohisi kwamba nimetulia kwa miaka kadhaa bila kubadili-badili utu wangu, basi nitafikiria kuanzisha urafiki wa kimapenzi.”
Kuna sababu nyingine kwa nini kuna hekima kusubiri. Biblia inatumia maneno “upeo wa ujana” kufafanua kipindi katika maisha ya mtu ambapo hisia za ngono na za kimahaba huanza kuwa na nguvu sana. (1 Wakorintho 7:36) Kuwa na uhusiano wa karibu na mtu mmoja tu wa jinsia tofauti unapokuwa na umri huo kunaweza kuchochea tamaa hizo na kuongoza katika mwenendo usiofaa.
Ni kweli huenda hilo lisiwe jambo zito kwa vijana wenzako. Huenda wengi wao wakawa na tamaa ya kufanya ngono. Lakini si lazima—wala hupaswi—kufikiri kama wao! (Waroma 12:2) Isitoshe, Biblia inatusihi ‘tuukimbie uasherati.’ (1 Wakorintho 6:18) Unaposubiri hadi upite upeo wa ujana, tunaweza ‘kuondolea mbali msiba.’—Mhubiri 11:10.

 Kwa nini nisubiri kabla ya kuanzisha urafiki wa kimapenzi?

Kuwa chini ya mkazo wa kuanzisha urafiki wa kimapenzi kabla ya kuwa tayari ni kama kulazimishwa kufanya mtihani wa somo ambalo umeanza tu kujifunza. Bila shaka, utahisi kwamba umeonewa! Unahitaji wakati wa kujifunza somo hilo ili uwe na habari zitakazokuwezesha kupita mtihani huo.
Ndivyo ilivyo pia kuhusiana na urafiki wa kimapenzi.
Urafiki wa kimapenzi si mchezo. Kwa hiyo, kabla ya kuwa tayari kumkazia fikira mtu mmoja hususa, unahitaji kujifunza “somo” muhimu—jinsi ya kujenga urafiki.
Baadaye, utakapompata mtu anayekufaa, utakuwa tayari kujenga urafiki wenye kudumu. Kusema kweli, ndoa nzuri ni muungano wa marafiki wawili wakubwa.
Kungoja muda upite kabla ya kuanzisha urafiki wa kimapenzi hakukunyimi uhuru. Badala yake, kunakupa uhuru zaidi wa ‘kushangilia katika ujana wako.’ (Mhubiri 11:9) Nawe utakuwa na wakati wa kujitayarisha kwa kuboresha utu wako, na zaidi ya yote, hali yako ya kiroho.—Maombolezo 3:27.
Kwa sasa, unaweza kufurahia kushirikiana na watu wa jinsia tofauti. Jinsi gani? Njia bora ni kushirikiana nao mkiwa katika vikundi vyenye mchanganyiko wa wavulana na wasichana ambavyo vinasimamiwa vizuri. Msichana anayeitwa Tammy anasema: “Nafikiri inafurahisha zaidi mambo yanapofanywa kwa njia hiyo. Ni afadhali kuwa na marafiki wengi.” Monica anakubaliana naye. Anasema: “Kushirikiana katika vikundi ni wazo zuri, kwa sababu unapata kuchangamana na watu wenye nyutu tofauti-tofauti.”
Kwa upande mwingine, ukimkazia fikira mtu mmoja tu mapema sana maishani, huenda ukavunjwa moyo. Kwa hiyo, usiwe na haraka. Tumia wakati huu wa maisha yako kujifunza jinsi ya kusitawisha na kudumisha urafiki. Baadaye, ukichagua kuanzisha urafiki wa kimapenzi, utakuwa umejifahamu vizuri zaidi na kufahamu sifa ambazo ungependa mwenzi wa ndoa awe nazo.

SABABU 5 KWANINI UPENDO HAUTOSHI KUJENGA MAHUSIANO BORA

\
Ukisoma kwa kutafakari makala hii utagundua kuwa kuweza kujifahamu sisi wenyewe vema, kuweza kujitawala sisi wenyewe, na pia kuweza ‘kuwasoma’ vema wenzi wetu , ni mambo ya msingi sana ili upendo tulionao uweze kudumisha mahusiano.  Msisitizo ni kwamba, pamoja na ukweli kuwa upendo ni kitu cha muhimu katika mahusiano, makala hii inaeleza kuwa kutegemea upendo pekee kama nguzo kuu ya mahusiano bora kunaweza kuwa jambo la hatari kwa mahusiano, kwa sababu zifuatazo:-
1. Binadamu ni kiumbe huru: Ni muhimu kukumbuka hili hasa kama unadhani kwakuwa unampenda fulani na umemuonyesha mapenzi yako yote basi hicho ni kama kifungo kwake kuwa hatoweza kutoka katika penzi lenu. Kwa asili binadamu ni huru, na anaweza kuamua kuutumia uhuru wake kufanya maamuzi mengine yoyote tofauti na unavyofikiri ni lazima afanye.  Kwa kuwa pia ni mbinafsi, basi kama upendo wako wote kwake hauendani na yale anayotazamia , unaweza kukuta ameshindwa kukaa katika penzi , ambalo kwa watu wengi wanaona kuwa ni penzi zito.
2. Binadamu ni mbinafsi kwa asili: Binadamu kwa asili huangalia maslahi yake kwanza kabla ya kuangalia ya mwingine. Mfano dhahiri wa ubinafsi huu ni pale inapotokea ajali , mara nyingi mtu huwaza kujiokoa mwenyewe kwanza kabla ya kufikiria wa karibu yake. Tumesikia habari za mama mzazi kuacha kitoto kichanga ndani wakati moto ukiendelea na yeye kutoka nje. Kuna habari pia za mama kumtumia mtoto wake kama ‘kifaa’ cha kuvunjia kioo cha gari , ili aweze kujiokoa, pale ambapo ajali ilitokea. Hivyo upendo tuu pekee hautoshi kumfanya mtu aendelee kukaa katika ndoa au mahusiano kabla ya ndoa (uchumba), ni muhimu yawepo mambo mengine yenye manufaa kwa mtu husika.
3. Binadamu ana mahitaji mengi  na yasiyo na kikomo:  Mwenza wako ana mahitaji mengi na yanaongezeka na kubadilika siku hadi siku kutegemeana na mabadiliko mbalimbali kama vile hali ya hewa, aina ya kazi,  watu anaokutana nao, mabadiliko ya teknolojia, mabadiliko ya kiuchumi n.k. Upendo wenu, hausimamishi mahitaji haya yasitokee, na kwamba upendo pekee hauwezi kuwa jibu la kutimiza mahitaji hayo. Inahitajika bidii katika kujituma kujiletea kipato, kuwa na mawasiliano bora kati yenu, kutambua mabadiliko na kuchukua hatua kabla mabadiliko hayajawabidilisha, na zaidi sana muweze kuwa na utamaduni wa kupanga mambo pamoja na kuwa waaminifu katika kutimiza yale mnayopanga. 
Chukulia mfano, wa wanandoa walioishi vema kwa miaka 5 ya ndoa, halafu ndoa ikaanza kulemaa kwa kuwa mmoja wao anaona hakuna uwajibikaji katika kumsaidia mwengine kujiendeleza kielimu, kibiashara, au kutimiza ndoto nyingine ambayo mwanandoa amekuwa nayo.
4. Binadamu wengi wanashindwa kujitawala:  Uwezo wa mtu kujitawala unaweza ukakinzana na upendo wake kwa mwenza wake, hivyo kuleta hali ya kutoridhika kwa mwenzi wake, kitu ambacho kinapunguza  au pengine hata kuondoa raha ya mahusiano. 
Mfano utakuta kwa kufuata makundi ya marafiki aliyonayo, mwanaume anakuwa mlevi wa kupindukia,  na kujikuta akiingia katika anasa na maamuzi mengine yasiyo mazuri kwa mpenzi wake na familia kwa ujumla. Hata hivyo mwanaume huyo huyo ukimuuliza kama anampenda mke wake au la, atakujibu anampenda sana. Tatizo nini ? Utajibiwa, ni pombe tuu ndio mmemtawala, na kwamba jamaa ana ‘kampani’ mbaya.
5. Maana isiyo sahihi ya upendo: Kuna wengi wanaodai wanao upendo lakini kiukweli walichonacho sio upendo bali ni tamaa au matakwa ya kuhitaji kutimiziwa mambo fulani. 
Maana halisi ya upendo sio vile unavyotaka fulani akufanyie mambo au jambo fulani, upendo sio vile unavyojisikia baada ya fulani kukutendea jambo uliloliona jema kwako, upendo sio vile fulani anavyokufanya ujisikie kwa sababu ya sura yake au umbo lake, BALI, upendo ni utayari wako wewe kufanya mambo yanayompendeza mwingine, kuwa tayari kuona mwingine ana furaha juu yako.  
 Kwa maana rahisi , upendo si jambo linalokuhusu wewe unajisikiaje, bali ni vile unavyotaka mwingine ajisikie.
Kwa maana nyingine, utatimiza vema upendo wako kwa kujitahidi kumfahamu mwenza wako, kutimiza yale anayohitaji (ili awe na furaha) sio kutimiza yale unayotaka wewe kwa makusudio yako binafsi. Upendo unahitaji kumheshimu mwenza wako, kumsikiliza, kumfanya akuamini, na aendelee kukuamini.
Pamoja na kuwa hisia za kimwili (chemistry) ni muhimu sana katika kujenga mahusiano yenu,  hisia za kimwili zisichanganywe na upendo. 
Kwakuwa fulani amekuvutia kimwili haina maana kuwa basi unampenda mtu huyo. 
Kufanya tendo la ndoa, sio lazima iwe ndio ishara ya uwepo wa upendo katika yenu, kwani wapo hata wanaofanya tendo la ndoa kama biashara.
Hitimisho
Mahusiano hususani mahusiano ya kimapenzi yanatutaka tuwe waajibikaji kwa wenzetu, na kwetu wenyewe. Kuwajibika kwa wenzetu ni pale tunapojifunza vya kutosha tabia,  na yale yanayompendeza na yasiyompendeza mwenza wetu. Wakati tunawajibika kwetu wenyewe kwa kujifunza kuhusu mapungufu yetu, na kujituma kujirekebisha. Mapenzi yanaleta majukumu, na bila kutambua na kutimiza majukumu husika, mara nyingi mapenzi yatageuka kuwa karaha, badala ya furaha.

Mambo ya kufanya kumzui mpenzi wako kutofanya mapenzi nawe


Kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi huwa ni furaha na kuchanganya pia. Unaingiwa na hisia ambazo hujawahi kuwa nazo na pia kupenda kwa dhati. Mpenzi wako anakufurahisha na wewe pia unamfurahusha. Lakini inaweza kutokezea sitofahamu wakati ambapo wewe hutaki ama hujiskii kufanya mapenzi lakini yeye akawa na hamu ya kufanya tendo hilo. Sababu zozote zile uko nazo, una haki ya kujizuia kutofanya tendo la ngono mpaka ile siku ambayo utajiskia kuwa umefikia siku yako. Mwili ni wako na maamuzi ni yako
1. Usilale kwake
Iwapo hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako, basi ni vizuri usijiingize katika hali ambazo zitachangia nyinyi wawili kuingiwa na hamu ya mapenzi. Iwapo umetoka deti na mpenzi wako, usijaribu kumsindikiza hadi kwake ama kuenda njia moja. Pia hutakiwi kuwa unazunguka sehemu ambazo mpenzi wako anaishi wakati kama huo kwa sababu inaweza kuchangia pakubwa kuingiwa na tamaa.
2. Usiwe mlevi
Kuna baadhi ya watu wanafikiria ya kuwa matumizi ya vinywaji ukiwa na mpenzi wako inapunguza hisia za kufanya mapenzi. Well, labda inaweza kuwa ni kweli lakini kulingana na utafiti ni kuwa mtu mlevi anapoteza mwelekeo wa kufanya maamuzi yafaayo. Hivyo ukiwa umeathirika na ulevi pamoja na mpenzi wako, kuna asilimia kubwa ya kufanya maamuzi ambayo si sawa.
3. Toa visababu ambavyo havitomkwanza mpenzi wako
Unaweza kutoa visababu kama vile unaumwa na kichwa, hujiskii vizuri nk. Ingawa kutumia uongo kwa mpenzi wako si jambo zuri, ni muhimu sana iwapo itakuja kwa maswala ya kufanya mapenzi ama kama hujiskii kufanya mambo mengine ambayo yanahusiana na wewe. Hivyo ni muhimu kupatia mambo mengine kipao mbele.

4. Fungua roho yako
Hii ndio njia nzuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi. Kukaa na mpenzi wako katika kikao na kumueleza ndani na nje kuhusiana na wewe kujizuia kutofanya mapenzi ni jambo nzuri zaidi kwa nyote wawili. Kumueleza ukweli mpenzi wako kutatoa ile nafasi ya kwako kuonekana kama unayapenda mahusiano yenu na hauhitaji kuficha ama kudanganya katika mahusiano yenu.
Iwapo atakubali basi itadhahirisha ya kuwa yeye anatilia maanani mahusiano yenu. Kama atakataa basi bila shaka mahusiano yenu hayatokuwa marefu.


ZITAMBUE CHANGAMOTO SITA (6) KWA KILA UCHUMBA/NDOA

Ukweli ni kuwa watu wawili wanapoamua kwa dhati kuwa katika mahusiano ni kwamba wanakuwa tayari katika akili zao wamejenga matarajio au matumaini ya kunufaika na uhusiano husika, hata kama hawawezi ambiana moja kwa moja kuwa “ aisee, mie kuwa na wewe nataraji moja , mbili, tatu….”.
Kunapokuwepo na upendo, basi pia kunaleta majukumu, ambapo bila ya kutimizwa kwa majukumu yanayotarajiwa kutimizwa, maana halisi ya mahusiano bora inapotea.
Hii si tuu kwa mahusiano ya kimapenzi, bali hata dini zinatufundisha kuwa Mungu anatupenda, na katika hilo, tunajukumu la kutii amri zake, na kwamba tusipotii amri zake, tunakuwa tumeharibu maana nzima ya upendo wake, kwani tutajikuta tumeingia motoni/jehanamu (Kinyume cha upendo).
Hata katika familia, tumesikia mzazi pamoja na upendo alioonyesha kwa mtoto wake toka yupo tumboni mpaka mtoto ameweza kujitegemea, endapo mtoto husika akashindwa kumjali ( hili ndio jukumu linalokuja na upendo wa mzazi), basi unaweza sikia mzazi huyo akitoa ‘laana’ au ‘akamwachia radhi’ mtoto wake mwenyewe wa kumzaa.
Ni wazi kuwa mara nyingi majukumu yanayoletwa na upendo huwa hayaelezwi wazi wazi, hata hivyo katika mahusiano, mambo yafuatayo yanaweza kuwa sehemu ya matarajio ambayo  wapenzi wanaweza kuwa makini ili waweze kuwapendeza wenzao. Kwa maana nyingine ni kuwa yafuatayo, ndio maeneo ambayo mtu aliye kwenye mahusiano ni muhimu ‘acheze’ vema ili kulinda mahusiano/penzi:-
Fedha:  Katika swala la fedha, jambo kubwa linalojitokeza ni namna ya kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya fedha.  Ni muhimu kuweka mikakati ya pamoja kwa mambo ya msingi kimaisha , na kila mmoja kutilia maanani mipango hiyo, kabla ya kuamua kutumia kipato chake kwa mambo ambayo pengine hayapo nje ya mipango ya kifedha ya wawili nyie kama wapenzi.  Bila shaka, kuendana na aina yenu ya kipato, aina yenu ya maisha, kama wapenzi mtakuwa na kiwango fulani cha fedha ambacho si busara mmoja wenu kuamua kutumia bila kumtaarifu mwenzake , hata kama matumizi husika ni muhimu sana, na haijalishi nani kazitafuta fedha husika.
Imani: Katika swala la imani, ni muhimu kufahamiana vema mwenendo wa kiimani wa mwenza wako, na kuheshimu kuwa swala hili ni nyeti, na mabadiliko ya kweli hayawezi kulazimishwa. Imani inaweza athiri namna mnavyoweza kuwasiliana kama wapenzi – kwani mwingine mwenye msimamo mkali wa kidini, anaweza kukataa jambo fulani hapo baadae, jambo ambalo pengine mwenza wake anaona ni jambo la kawaida tuu. Imani inaathiri malezi ya watoto, na inaweza athiri shughuli za kiuchumi za wawili nyie, mfano pale mmoja wenu anapoamua kujikita katika  ‘huduma’ zaidi, kuliko familia na shughuli za kuingiza kipato.
Mahali pa kuishi:  Mtaa gani , wilaya gani, mkoani gani, nchi gani au bara gani kila mmoja wenu anatazamia muishi ni jambo la msingi kuliweka wazi kati yenu. Jambo hili linaweza kuendana na mambo mengine mengi ambayo yanachochea mabadiliko ya muda mfupi na hata muda mrefu katika maisha yenu, kama vile , aina ya kazi mnazotarajia kila mmoja wenu kufanya, na aina ya kazi unazotamani au kufikiri ni vema mwenza wako afanye.
Watoto: Hili ni jambo zito haswa katika vipengele vya lini watoto wapatikane (ujauzito), idadi ya watoto, aina ya malezi kwa watoto watakaopatikana, na zaidi sana majukumu ya kifedha katika malezi ya watoto (mfano, nani atalipa ada ya shule, n.k). Pamoja na kutafakari hayo, watu wawili mlio katika mahusiano, ni muhimu mkatengeneza picha ya maisha ya watoto wenu endapo mmoja wenu atatangulia mbele za haki (atafariki), na hata ikiwezekana  mwaweza fikiria na kupanga aina ya maisha mnayotaka watoto wenu waishi pale nyote wawili hamtokuwepo  duniani. Inapotokea mambo kama hayo yaliyotajwa hapo juu hayajawekwa wazi mbele yenu, ni rahisi mmoja wenu kufanya mambo yasiyompendeza mwengine –mfano wakati mwingine anafikiria akiba ya baadae ya watoto ili wakasome international school, mwingine anafikiria namna ya kutanua ili ‘kuuza sura’.
Falsafa ya maisha:  Swala hili linahusu wa kipekee na tafakari huru ya kila mmoja wenu kuhusu mambo kadhaa ya kimaisha kama vile mtazamo wa kila mmoja wenu kuhusu biashara (mwingine biashara ni kitu cha kuweka heshima kwa jamii, wakati mwingine biashara ni kielelezo cha huduma kwa jamii na hivyo kinahitaji muendelezo).
Falsafa pia inahusu namna kila mmoja wenu anavyochukulia mambo kama vile kusaidia watu wengine,  kuwa na mahusiano na watu wa jinsia tofauti (wapo wasiotaka hata classmet ampigie simu mpenzi wake). Falsafa pia inahusika na namna kila mmoja anavyotafsiri mafanikio katika maisha, na alivyo tayari kufanya yanayopaswa kufanywa kufikia mafanikio (Mfano, wengine mafanikio ni mali na umaarufu, wakati kwa wengine mafanikio ni namna anavyoweza kuwa na furaha na uhuru , pamoja na kusaidia wengine).
Katika juhudi za kufikia mafanikio unawea kukuta wapenzi mnatofautiana kwani mmoja anaweza amini rushwa ndio suluhisho pekee la kufikia anakotaka, wakati mwingine anaamini tofauti na hivyo.  
Hisia za kimapenzi: Ni jambo la msingi kutokupuuzia hisia za kimapenzi za kila mmoja wenu. Tambua vile mwenzako angependa akuone unamvutia na vile ambavyo unamjali hisia zake. Ni kweli kuwa katika mahusiano, hisia za kimapenzi zinaweza zisichukue nafasi kubwa kati yenu kwani kuna mambo mengi ya kufanya pamoja kama wapenzi, hata hivyo pamoja na udogo wake wa muda, jambo hili nyeti lisipopewa kipaumbele, linaweza sababisha mengine yote kuharibika. Zaidi sana, kumbuka wewe na mpenzi wako, ni watu wa jinsia mbili tofauti, kinachowafanya muungane kiasili ni hizo hisia za mapenzi kati yenu.
Hitimisho: Sio lazima kama watu wawili mlio katika mahusiano muwe na mtazamo sawa katika hayo yote yaliyoelezwa hapo juu, hata hivyo, ni muhimu sana kwenu nyote kuwa na picha kichwani ya mtazamo wa mwenza wako kuhusu mambo hayo niliyotaja hapo juu.
Pale mnapokubaliana kutofautiana katika mambo yaliyotajwa hapo juu (mf.mambo ya fedha, na imani), hakikisheni mnakubaliana bila kutofautiana kuhusu athari za kutofautiana kwenu, na jukumu la kukubali athari hizo kwa mahusiano yenu.


HATUA 3 ZA KUBADILI TABIA INAYOKUKWAZA KATIKA MAHUSIANO

Kati ya kitu ambacho kinasumbua wengi na kimekwamisha wengi ni tabia.Wengi wana huzuni ndoa zimewashinda,kazi zimewashinda,fedha na mafanikio vimewakimbia,watoto wamewashinda,hawana marafiki hata miili yao haina afya kwa sababu ya tabia tu.
Wengine wamejiona ni kama wana laana,wengine wanafikiri labda wanaugua ugonjwa flani lakini shida siyo shida nitabia zao tu.
Hebu tuone namna gani tunaweza badilika au kubadilisha tabia zetu.

Tafuta Kujijua Binafsi:
Jiulize kwa nini umekuwa ukikwama mara kwa mara katika eneo  flani kama vile:-

(a)Kwanini haudumu ktk mahusiano ya kirafiki au ya mapenzi.
(b)Kwanini umeshindwa kufanikiwa kimaisha.
(c)kwanini watu wanakuchukia.
(d)kwanini hau-dumu kwenye kazi.
Unaweza pia kumuuliza mtu unaye mwamini akwambie jinsi ulivyo.

Chukua Hatua Kubadili Tabia:
Anza kufanya kinyume na ulivyokuwa umezoea kwa maana ya kwamba yale ambayo ni mazuri sasa. Zingatia haya:-
(a)Wataalam wa mambo wanasema ili jambo liwe tabia linafaa kufanya kwa siku “21” bila kuacha  baada yah apo jambo hilo litakuwa tabia.
(b)Ikikubidi kubadilisha mazingira ambayo unahisi ndiyo yamekuharibia tabia badisha hata kama itakugharimu.
(c)Ikikubidi kubadili marafiki ambao wamekuwa wakikushauri vibaya achana nao tu utapata marafiki wengine.
Majumuisho
Kumbuka haya:
(a)Tabia inaundwa au inatengenezwa na tabia ya mtu inamtegemea mtu mwenyewe na maamuzi yake.
(b)Tabia yako inaweza kukukwamisha kabisa katika Maisha yako yote au kukufanikisha katika mambo yote.
(d)Tabia yako itakutenga na watu au itakuunganisha na watu.
SASA UAMUZI NI WAKWAKO KUTENGENEZA TABIA YAKO ILI WATOTO WAKO WAIGE MEMA KUTOKA KWAKO.

MADHAIFU MATANO (5) YANAYODIDIMIZA MAHUSIANO NA NDOA


Makala hii ni tafakari huru kuhusu mambo ya msingi katika mahusiano.  Hapa utapata tafakari ya maana ya maneno na imani ambazo zinatutatiza wengi wetu.
1. Mchanganyiko mkubwa kuhusu maana ya mahusiano, mapenzi na ndoa:
Labda kipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini yasiwepo mahusiano wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndio ukweli wenyewe.  Ndoa ni namna tuu ambayo wawili walio kwenye mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa wao wapo rasmi katika mahusiano. 
Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namna ya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokea kuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo za ndoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawana mali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwa Mungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua.
 Hivyo basi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi. Kiuhalisi inabidi kwanza yawepo mahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume cha hivyo ni kuwa unakula kiapo ‘feki’.
Ndio maana basi, ni muhimu kwa wapenzi kutambua kweli kama wanahitajiana, kuwa kwenye mahusiano na kutafakari kwa uhuru kama kweli wanataka kuweka kiapo rasmi cha kuwa pamoja.
Kutumia ndoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni maamuzi magumu ambayo pengine yanaweza yasilete faida hapo baadae.
2.Mahusiano na ndoa nyingi huyumbishwa na Matarajio yasiyo halisi
Kabla hata ya kuingia katika mahusiano na hatimaye ndoa wengi wetu huwa na matarajio binafsi ya kimaisha. Matarajio haya yanajumuisha vile tunavyotaka sie wenyewe kuwa hapo baadae, pamoja na matarajio ya vile tunavyotaka wenza wetu wawe.
Hata hivyo katika hali halisi tunajikuta sisi wenyewe hatuwezi kujibadilisha au kujiweka kwa usahihi vile tunavyotamani kuwa (kwa sababu kwa kila tunachojaribu kufanya kuwa bora, tunajikuta bado tuna madhaifu mawili matatu). Pamoja na ukweli huu, tunajikuta tupo na matarajio ya kuwafanya wenza wetu wawe watu wa aina fulani. Kwakuwa kiasili binadamu ni kiumbe huru, tunajikuta wenza wetu nao wakiwa ‘busy’ kutimiza ndoto za vile wanavyotamani kuwa iwe kimavazi, aina ya marafiki, utafutaji wa kazi , kujiendeleza kimasomo, aina ya mali za kununua, hata kufikiria tofauti aina ya maisha wanayotaka muishi.
Matokeo yake ukinzani huu wa matarajio ni mkanganyiko wa mgongano wa mawazo kati ya wawili nyie, na mwanzo wa vita ya chini kwa chini ya nguvu ya maamuzi katika mahusiano yenu.
3. Kuweza kumbadili tabia mwenza wako
Mojawapo ya jambo ambalo hufanywa na wengi walio katika mahusiano ni kuwa na ‘tamaa’ ya kutaka kumbadili tabia fulani mwenza wake. Hata hivyo ‘tamaa’ hii ni sehemu ya yale tunayoyaita matarajio yasiyo halisi, kwani tabia ya mtu hujengwa na mambo mengi sana, ikijumuisha aina ya makuzi, aina ya mfumo wa imani mtu anaouamini, aina ya marafiki alio nao, uwezo wake wa kujiamini katika kubadili tabia kwani wengine wameshakata tamaa kuwa hawawezi kukata tamaa, na zaidi sana, mabadiliko ya tabia huhitaji mfumo endelevu na wenye kusoma vema asili ya tabia ili kuweza kuirekebisha.
Hata hivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea ‘mapenzi’au vitisho tuu kama vile ‘nitakuacha mie ’,  kama sababu ya kumfanya mtu abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili ya tabia ya mtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya zoezi la kubadilishana tabia kuwa gumu na pengine lisilowezakana.
4. Kuvumilia ndio kuonyesha upendo na ndio kudumisha mahusiano
Hii ni aina nyingine ya matarajio ambayo sio halisi kwani kiukweli kila mtu analo jukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba ‘uzembe’ wa mwingine kwa kisingizio tuu cha kuwa unaonyesha upendo hususani pale ambapo ni kwa uzembe tuu au kutokujali kwake mwenza husika amefanya jambo fulani.
Kwa jinsi kasumba hii ilivyo enea sio ajabu kukuta mtu akifanya mambo mabaya kwa mwenza wake kwa makusudi ili tuu eti apime kama kweli mwenza wake ni mvumilivu.
Kumbuka hapa hatumaanishi kuwa kusamehe ni kosa. Hapana, kusameheana ni muhimu, lakini sio kwamba ni muhimu tuu katika mapenzi. Kusameheana ni jambo la asili, na tunapaswa kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano. 
Tunachosema ni kuwa kuna  kasumba ya baadhi yetu kuona kuwa wanayo ‘haki’ ya msingi ya kukosea eti tuu kwakuwa tuu mwenza wake analazimika kusamehe ili kuonyesha kweli anao upendo wa dhati.
Amini usiamini, kasumba hii ya kutarajia aina ya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio tuu cha kuwa upo kwenye mapenzi na mwenza wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwani mwenzi wako nae ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha, isitoshe na yeye anahitaji upendo na kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia kwako kusamehewa na kuvumiliwa kuna mnyima haki mwenza wako. Hatimaye kutegema kwako kusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie mashaka upendo wako kwake.
5. Uaminifu = Upendo= Kudumu kwa mahusiano
Pamoja na ukweli kuwa mwenza wako anatarajia utakuwa muanifu kwake, elewa kuwa kuwa mwaminifu pekee katika mahusiano yako sio tiketi ya kudumu kwa mahusiano yenu kwakuwa watu wanaingia kwenye mahusiano sio tuu kwa kuwa wanataka kuwa na mtu mmoja muaminifu bali wana mahitaji mengine wanayohitaji.
Zungumza na mwenza wako, fanya utafiti wako binafsi kuhusu mpenzi wako ujue mambo mengine anayohitaji toka kwako. 
Pia msikilize anapokutaka urekebishe mambo kadhaa au ufanye mambo fulani. Inapendeza pale unapomfanyia mtu mambo yanayompendezesha kwa kuwa hivyo ndivyo anavyotaka, sio kwakuwa tuu wewe unadhani kufanya hivyo kutampendezesha mhusika.

FANYA HAYA 6 KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU

Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.  Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.
1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:  Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
2. Upekee wa mambo:  Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.
3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua. 
4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza  kuzitumia kupata suluhu ya tatizo. 
5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa  nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine. 
6. Kuweni peke yenu:
Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni  kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi.  Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao  kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.
7. Nenda ‘darasani’ :  Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu. Mfano wa makala unazoweza kusoma ni kama vile:

Monday, January 23, 2017

YAFAHAMU MAHUSIANO


Siku zote mapenzi huyapa maisha thamani lakini wapo ambao hujikuta kwa namna moja ama nyingine wanatengana na wapenzi wao kwa sababu tu ya mihangaiko ya kila siku ya kujitafutia riziki. Masomo na wakati mwingine utengano huwa ni matokeo ya wapendanao kuishi sehemu tofauti. Hii huwakumba sana wanafunzi wa vyuo na shule za bweni (hostel).

Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa, Hata hivyo, mapenzi ya mbali huna ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama anakofanyia kazi laazizi na mwandani wake.
Pamoja na hayo yote bado umbali hauwezi kuwa ni tatizo kubwa sana la kutetelesha uhusiano wako na mpenzi wako. Mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya haya.

MAWASILIANO MARA KWA MARA.
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.

Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliye mbali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe.

HESHIMU HISIA ZAKO

Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi, Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.

Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake (lakini sio ule wakubomoa!) Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonesha unampenda.

UMBALI ISIWE KIGEZO KUNYIMANA.
Mpe mwandani wako raha kamili kama ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila shaka unajiuliza inawezekanaje? Hili linawezekana kwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano. Mfano kama nyote mna simu jiandae vya kutosha nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu ambayo utakuwa huru kuongea ama kufanya chochote Kitakachokufanya uhisi raha isiyo na kifani na kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro bila kutarajia.

Bila shaka kila mtu anamfahamu vema mpenzi wake na hasa nini hupenda kufanyiwa ili awezekufika safari yake na kama ndivyo basi hakikisha unafanya mambo yote ambayo ukimfanyia mwenzi wako pindi mnapokuwa kwenye mambo fulani hupagawa.