YAFAHAMU MAHUSIANO
Siku zote mapenzi huyapa maisha thamani lakini wapo ambao hujikuta kwa
namna moja ama nyingine wanatengana na wapenzi wao kwa sababu tu ya
mihangaiko ya kila siku ya kujitafutia riziki. Masomo na wakati mwingine
utengano huwa ni matokeo ya wapendanao kuishi sehemu tofauti. Hii
huwakumba sana wanafunzi wa vyuo na shule za bweni (hostel).
Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao
hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote
itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa, Hata hivyo, mapenzi
ya mbali huna ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya
dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa
muhanga kwa kuamia anakoishi ama anakofanyia kazi laazizi na mwandani
wake.
Pamoja na hayo yote bado umbali
hauwezi kuwa ni tatizo kubwa sana la kutetelesha uhusiano wako na
mpenzi wako. Mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya
haya.
MAWASILIANO MARA KWA MARA.
Mawasiliano
ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi
uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una
mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia
ama sms, email, kadi au simu.
Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote
ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo
kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi
kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliye mbali anapokutumia
ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo
kuuchuna hadi ulalamikiwe.
HESHIMU HISIA ZAKO
Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya
wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe
na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi, Kama kweli
unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za
kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi
mtakapokutana tena.
Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza
wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu
wa hapa na pale mwenzi wake (lakini sio ule wakubomoa!) Hivyo heshimu
hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonesha unampenda.
UMBALI ISIWE KIGEZO KUNYIMANA.
Mpe
mwandani wako raha kamili kama ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila
shaka unajiuliza inawezekanaje? Hili linawezekana kwa kutumia njia
yoyote ya mawasiliano. Mfano kama nyote mna simu jiandae vya kutosha
nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu ambayo utakuwa huru kuongea ama
kufanya chochote Kitakachokufanya uhisi raha isiyo na kifani na
kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro bila kutarajia.
Bila shaka kila mtu anamfahamu vema mpenzi wake na hasa nini hupenda
kufanyiwa ili awezekufika safari yake na kama ndivyo basi hakikisha
unafanya mambo yote ambayo ukimfanyia mwenzi wako pindi mnapokuwa kwenye
mambo fulani hupagawa.
No comments:
Post a Comment