Mwanamke akipenda anapenda kweli!
Mwanamke akikupenda anakuwa na furaha, anakuwa anajivunia kuwa na wewe, na hujihisi furaha kuongea na wewe.
Hupenda awe rafiki wa rafiki zako na ndugu zako, uvipendavyo na yeye
atavipenda, atabadilisha mtindo wake wa maisha kuendana na mtindo wako.
Haitajalisha ni kiasi gani utamuudhi, atakusamehe hata kabla
hujamuomba msamaha, atachokifanya ni kusubiri tu umuombe msamaha
kuthibitisha kama kweli umejutia kosa lako.
Atajaribu kuwa na wivu na atakulinda kwani atahitaji uwe wake, wake
peke yake na sio ku share. Atawakataa wengine wote wanaomtongoza kwa
sababu ameona kesho yake ipo mikononi mwako.
Haitajalisha ni kiasi gani uko mbali na yeye, atajilinda kwa ajili
yako. Atalike na ku comment kila kitu unachoweka facebook hata kama ni
cha kipuuzi (hahaahaa).
Atakujibu kwa wakati text zako either watsapp, za kawaida au inbox ya
fb. Hatajali kama unampa pesa au laa, kama ni tajiri au laa kwa sababu
lengo lake ni kujenga maisha na wewe na sio kupass time ameona
potentials kwako.
Atakuonyesha marafiki zake na ndugu zake, kwa sababu anajivunia kuwa mpenzi wako.
Tafadhali sana, muangalie mwanamke huyo, moyo wake umejawa na mapenzi, anastahili kutunzwa na kupendwa kama almasi.
Lakini tatizo kubwa la hawa "wavulana" (baadhi yao) baada ya kumfanya
akupende zaidi, baada ya kupoteza muda wake juu yako, baada ya
kuwakataa wanaume wengine ambapo kimsingi wengine walikuwa tayari
kumuoa, baada ya kumuacha akutambulishe kwa ndugu zake na marafiki sasa
unamuacha, unamkataa kwa mbwembwe nyingi, unamuacha akiwa na maumivu na
aibu kubwa kwamba atawaambia nini wazazi wake, ndugu na marafiki,
atatambulisha wangapi?
Na akiulizwa yuko wapi yule uliyetutambulisha? Awajibu nini!? Ofcoz
atakachofanya ni kuinamisha kichwa huku ameshika mashavu! Hana jibu ni
aibu na maumivu makubwa kwa kuwa alikupenda kwa dhati.
Mbona mnawaweka katika wakati mgumu wanawake waliopewa moyo wa kupenda?
Brothers, usimfanye mwanamke wako ajute kwanini alipenda, usifanye
wengine wamcheke na kumdhihaki. Timiza ahadi yako, kama amekukosea na
kukuomba msamaha jaribu kumpa nafasi ya pili. Kila mtu anahitaji nafasi
ya pili ili aweze kurekebisha pale alipokosea.
Na nyie vijamaa mnaokua sasa, miaka 14 na kuendelea msiige tabia ya
sisi kaka zenu, hiyo sio tabia njema kabisa. Jifunzeni kuheshimu hisia
za mtu. Kujeruhiwa kihisia kunauma kuliko maumivu ya risasi.
Kama huna future nae usimtongoze na kumpa mimba
No comments:
Post a Comment